Chama alamba Sh 1 Milioni

Tuesday May 04 2021
tuzo pic
By Oliver Albert
By Thobias Sebastian

Kiungo Wa Simba, Clatous Chama amekabidhiwa tuzo na sh 1 Milioni na kampuni ya Emirate Aluminium profile baada ya kuibuka mchezaji bora Wa mashabiki Wa  mwezi April.
Mashabiki Wa Simba hupata fursa ya kuchagua mchezaji bora kila mwezi tangu tuzo hiyo ilipoanzishwa mwezi April.
Chama ameibuka mshindi baada ya kuwashinda washindani wake Kipa Aishi Manula na beki Shomari Kapombe.
Chama amesema tuzo hiyo imempa motisha ya kufanya vizuri zaidi kwa ajili ya timu na kupata tuzo nyingine.
"Nawashukuru sana mashabiki kwa kutambua mchango wangu na kunipigia kura nyingi kuwa mchezaji bora Wa mwezi.
"Tuzo hii naipeleka kwa wachezaji wenzangu ambao tumekuwa tukishirikiana uwanjani kwa ajili ya mafanikio ya timu na itakuwa chachu ya mimi kuendelea kujituma zaidi ," amesema Chama.
Chama amesema wataendelea kupambana uwanjani kwa ajili ya timu ili kupata matokeo mazuri yatakayowapa furaha mashabiki Wa klabu hiyo.

Advertisement