Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chama afunguka, kutua Dar kesho

KIUNGO fundi wa Simba, Clatous Chama anatarajiwa kurejea nchini kesho Juni 10 mchana ili kuungana na wachezaji wenzake kwa maandalizi ya mechi za mwisho za Ligi Kuu Bara.
Chama aliondoka nchini wiki kadhaa kwa mapumziko mafupi sambamba na kujiuguza jeraha alililonalo na kumaliza matatizo ya kifamilia aliyokuwa nayo, ikiwamo kwenda kuadhimisha mwaka mmoja wa kumbukumbu ya kifo cha mkewe, Mercy Chama aliyefariki dunia Mei 29, 2021.
Kiungo huyo aliyerejeshwa nchini kutoka RS Berkane ya Morocco katika dirisha dogo baada ya timu hiyo kumsajili awali mwishoni mwa msimu uliopita, aliondolewa kikosi cha Simba siku chache kabla ya mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Yanga.
Chama ameliambia Mwanaspoti kuwa, kesho (Ijumaa) Mchana atarejea nchini na moja kwa moja ataenda kambini kujiunga na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mechi tano zilizobaki kukamilisha msimu huu.
Kiungo huyo tangu arejee Msimbazi amefunga mabao manne na kuasisti moja katika ASFC, huku kwenye Ligi Kuu amefunga mabao matatu, licha ya kushindwa kutumika mara kwa mara chini ya Kocha Pablo Franco aliyetupiwa virago vyake Simba hivi karibuni.
Msimu uliopita, Chama akishirikiana na Luis Miquissone anayekipiga Al Ahly ya Misri waliiongoza Simba kutetea taji la Ligi Kuu kwa msimu wa nne mfululizo na Kombe la ASFC kwa mara ya pili, mbali na kuifikisha timu hiyo robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.