CAF yaridhia kumchagua tena Infantino

CAF yaridhia kumchagua tena Infantino

ARUSHA. Wajumbe wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kwa pamoja wameridhia kumuunga mkono Rais wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA), Gianni Infantino katika uchaguzi mkuu ujao.

Wajumbe hao wameridhia hayo katika mkutano mkuu wa CAF ambao unafanyika katika ukumbi wa mikutano ya Kimataifa ya Arusha "AICC" .

Mkutano huo unahusisha wajumbe 156  kutoka nchi 52 wanachama CAF kati ya nchi 154 huku Kenya na Zimbabwe hazijashiriki mkutano huo kutokana na kufungiwa na FIFA.

Mkutano huo umehudhuriwa na zaidi wa watu 400 kutoka mataifa mbalimbali akiwemo Rais wa FIFA, Gianni Infantino, Rais wa Soka Qatar (QFA), Sheikh Ahmad Thani na waziri mkuu, Kassim Majaliwa wengine wengi.