CAF yaipokonya Guinea haki ya kuandaa Afcon 2025

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limefungua upya maombi ya kuandaa Afcon 2025 baada ya kuipokonya Guinea haki hiyo.

Kuondolewa kwa haki hizo kulifuatiwa mkutano uliofanyika Ijumaa iliyopita mjini Conakry kati ya rais wa mpito wa Guinea, Kanali Mamady Doumbouya, na Rais wa CAF Patrice Motsepe.

Motsepe alitaja miundombinu na vifaa nchini Guinea kuwa haviko tayari kuandaa mashindano ya kimataifa ya Afcon.

Bosi huyo wa CAF ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Caf, Veron Mosengo-Omba alisema kama alivyonukuliwa na tovuti ya CAF; “Nimetembelea Guinea leo [Ijumaa] kwa heshima ya watu wa Guinea ili kujadili nia ya CAF ya kushauri na kufanya kazi pamoja na wadau wa soka kujenga na kujenga miundombinu na vifaa vya soka hapa nchini,"

“Hii itaiwezesha Guinea kujinadi na mataifa mengine yanayoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (CHAN) yatakayofanyika baada ya CHAN itakayoandaliwa na Algeria mwaka 2023, kwa kuzingatia uamuzi wa CAF wa kutoendelea na Afcon 2025. Guinea.”

Kufuatia kikao cha Kamati ya Utendaji siku ya Jumamosi, CAF imeamua kufungua tena zabuni hiyo.

"Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) (EXCO) ilikutana Jumamosi Oktoba 1, 2022 huko Algiers, Algeria na kutangaza kufungua tena zabuni za Kombe la Mataifa ya Afrika la TotalEnergies 2025," taarifa ya shirika la soka

Hiyo siyo mara ya kwanza kwa nchi kufungiwa kuandaa Afcon. Cameroon ilipokonywa haki ya kuandaa mashindano ya 2019 kwa sababu hawakuwa tayari lakini walitunukiwa mashindano ya 2021 ambayo yalifanyika mapema mwaka huu kwa sababu ya kuchelewa kulikosababishwa na janga la Covid-19.

Hata hivyo Morocco na Algeria zimeripotiwa kuwasilisha maombi yao ya kuandaa michuano hiyo.