Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cadena anajua chakufanya Simba

Muktasari:

  • Simba wanaondoka nchini alhamisi kuwafuata Jwaneng Galax ya Botswana mchezo utakaopigwa Jumamosi na baada ya hapo watakuwa wageni wa Wydad AC, Desemba 9.

KAIMU kocha mkuu wa Simba, Daniel Cadena amesema wana mlima mrefu kwenye dakika 180 za ligi ya mabigwa hatua ya makundi ugenini huku akisisitiza kuwa wamejiandaa kushindana na sio kushiriki.

Simba wanaondoka nchini alhamisi kuwafuata Jwaneng Galax ya Botswana mchezo utakaopigwa Jumamosi na baada ya hapo watakuwa wageni wa Wydad AC, Desemba 9.

Akizungumza na Mwanaspoti, Cadena alisema wanatambua wanapitia nyakati ngumu kutokana na timu kukosa matokeo mazuri hivi karibuni lakini hilo haliwaondoi kuwa wanatakiwa kushindana ili waweze kufikia malengo.

“Tunapitia nyakati ngumu ni sehemu ya matokeo kwenye soka hilo halitufanyi tukashindwa kujiweka katika mazingira mazuri ya ushindani tunaendelea nja maandalizi na timu itaondoka Alhamisi;

“Tuna mlima mrefu wa kupanda kwenye dakika 180 ugenini lengo ni kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi kwenye mechi hizo kama saisi tumekubali kupoteza pointi mbili nyumbani tunatakiwa kutumia vyema uwanja wa ugenini ili kuirudisha timu kwenye ubora japo sio rahisi,” alisema.

Cadena aliupongeza uongozi kwa kutenga muda wao na kuzungumza na wachezaji wake ili kufahamu shida ilipo huku akisisaitiza kuwa njia iliyotumika ni sahihi itaweza kuwarudisha wachezaji mchezoni.

“Tunaenda kukutana na timu ambayo imetoka kutumia vyema uwanja wa ugenini ikisahindea haitakuwa rahisi na tukimalizana na hiyo timu tunaenda kukutanba na timu ambayo imepoteza mchezo wake wa kwanza nyumbani tunahitaji maandalizi mazuri;

“Wachezaji wangu wamekiri pia kuumizwa na matokeo mabaya wanayoyapata na kuaahidi kufanya vizuri kwenye mechi zilizo mbele yetu mbele ya viongozi na kuwaomba mashabiki kuwa na utulivu hii ni nzuri kisaikolojia.” alisema. Simba ambayo ipo kundi B sambamba na Jwaneng anayeongoza kundi na pointi tatu baada ya kushinda ugenini, Asec Mimosas na Wydad AC wanaburuza mkia baada ya kukubali kichapo nyumbani.