Burundi, Uganda wakomaliana dakika 45

MECHI ya kumtafuta mshindi wa tatu wa michuano ya Challenji kwa Wanawake kati ya Uganda na Burundi imekwenda mapumziko bila kufungana.
Mchezo huo uliokuwa na ushindani kila timu ikicheza kwa akili, ufundi na mbinu huku akimsoma mwenzake ilisababisha timu hizo kwenda katika mapumziko hayo bila kufungana.
Uganda walianza mashindano haya kwa kasi kutokana na kushinda mechi zote za makundi. Ilitegemewa kumaliza mchezo huo mapema kwa sababu ya ubora wao lakini katika mechi imekuwa ngumu.
Washambuliaji wao Nalukenge Juliet,  Najjemba Fauzia na Ikwaput Fadhila walizidiwa ujanja na mabeki wa Burundi Keza Angelique, Uwineza Djazila na Bukuru Rachel kila walipopandisha mashambulizi waliwazidi.
Kocha wa Uganda,  Faridah Belega alifanya mabadiliko kwa kumtoa Ikwaput nafasi yake ikachukuliwa na Nababi Amina kuona namna gani anapita.
Timu kutoka mataifa nane ya Afrika Mashariki na Kati zilishiriki michuano hiyo ambazo ni Tanzania Bara, Uganda, Kenya, Burundi, Zanzibar, Djibouti, Sudan Kusini na Ethiopia.