Bocco, Nyoni kuikosa Namibia leo

TAIFA Stars inajiandaa kukabiliana na Namibia leo usiku wa saa 4:00, Uwanja wa Limbe nchini Cameroon, huku ikiwakosa wachezaji watatu ambao ni John Bocco (nahodha), Erasto Nyoni na Ibrahim Ame.

Wachezaji hao wapo chini ya uangalizi wa madaktari, kutokana na kusumbuliwa na majeraha, hivyo watauushuhudia mchezo huo wa pili kwa Stars wakiwa jukwaani.

Mchezo huo ni muhimu kwa Stars kushinda, baada ya kupigwa mabao 2-0 katika  mechi ya ufunguzi dhidi ya Zambia.

Beki wa timu hiyo, Shomary Kapombe mara baada ya kumaliza dakika 90 za mechi ya kwanza na Zambia, alikaririwa akisema kipindi cha kwanza walicheza vizuri, kilichowaangusha ni dakika 45 za mwisho kushinda kumiliki mipira.

Huku akijipa matumaini ya mchezo wa leo, kwamba ndio unaotakiwa kuangaziwa zaidi baada ya ule wa kwanza kupoteza.
"Kipindi cha kwanza tulicheza vyema, lakini cha pili wapinzani wetu waliutawala mchezo," mwisho wa kunukuu.