Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki Mbao ajipeleke kwa KMC kimtindo

Muktasari:

  • Beki huyo amesema ana ofa nyingi pamoja na KMC, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar na JKT Tanzania

Dar es Salaam. Beki wa Mbao FC, Amos Charles anawindwa na KMC inayotegeneza kikosi chake kwa msimu mpya wa Ligi Kuu sambamba na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Beki Charles amemaliza mkataba wake na Mbao FC mwishoni mwa msimu ameweka wazi kuwa hadi sasa anaofa nne mkononi mwake.

Charles alisema anamshukuru Mungu amecheza kwa mafanikio Mbao na kutengeneza jina anachokipambania sasa ni kuhakikisha anapata timu bora zaidi.

"Ni ofa nyingi pamoja na KMC, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar na JKT Tanzania hizi ni timu ambazo tayari nimeshakaa nazo mezani kuna nyingine nimefanya nazo mawasiliano tu kwa njia ya simu sifahamu kama zinamaanisha au la,"

"Kuhusiana na dau langu ni bei gani kwa timu inayohitaji huduma yangu naomba ibaki kuwa siri ya klabu yangu nitakayoingia nayo mkataba na mimi mwenyewe kikubwa ni kusubiri ni timu gani kati ya hizo itakubaliana na dau nililoliweka mezani,"alisema Charles.