Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki Azam atua mezani Simba


BEKI wa Azam FC, Nathaniel Chilambo ana asilimia kubwa ya kutua Simba msimu wa ujao, akiwa hadi sasa hajasaini mkataba mpya na matajiri hao wa Chamazi.


Beki huyo amekuwa akiwindwa na Simba kwenye kila kipindi cha usajili, lakini sasa inaonekana kuwa yupo kwenye wakati mzuri wa kutua kwenye timu hiyo kwa bado hajakubali kusaini mkataba mpya na timu hiyo ambayo kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Chilambo mkataba wake wa sasa wa kuendelea kusalia mitaa ya Chamazi unamalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo unafungua mlango kwake kuzungumza na timu nyingine na inaelezwa kuwa tayari ameshakaa mezani na Simba na kuweka mipango sawa.

Taarifa za ndani kutoka Simba zinadai kuwa beki huyo tayari ameshasaini mkataba wa awali wa miaka mitatu kujiunga na Simba kama mchezaji huru kwa ajili ya msimu ujao wa 2026/2027, ikiwa timu hiyo inaendelea kujiimarisha kwa ajili ya ligi na michuano ya kimataifa msimu ujao.

"Mazungumzo na usajili wa awali yalikamilika tangu mapema mwezi Mei na makubaliano kamili yanatarajiwa kufungwa hivi karibuni baada ya msimu wa ligi kukamilika kwa kuwa sasa bado anaitumikia timu nyingine hatuwezi kuweka kila kitu wazi tutakuwa hatuna heshima," kilidai chanzo hicho.


HESABU ZA SIMBA

Simba imeanza kusaka mbadala wa Shomari Kapombe ambaye amekuwa kwenye nafasi hiyo kwa muda mrefu, akionyesha kiwango bora kwenye kila mchezo ambao amecheza.

Taarifa za ndani zilisema kuwa;" Uongozi wa Simba unamchukulia Chilambo kama mchezaji sahihi wa muda mrefu wa kusaidiana na beki mkongwe Shomari Kapombe ambaye amekuwa akikosa msaidizi sahihi wakati akiwa anaumwa au kupumzishwa kwenye kikosi hicho.

"Kazi yake nyingine ni kuongeza ushindani na nguvu kubwa upande wa kulia wa ulinzi, ambapo atachuana vikali namba moja na Kapombe pamoja na David Kameta 'Duchu' ambaye bado hana uhakika wa kusalia klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu."

Chilambo ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani (ikiwemo beki wa kushoto na kiungo mkabaji) hii itampa wigo mpana kocha katika kupanga mifumo ya kiulinzi msimu ujao.

Nafasi ya Chilambo ndani ya kikosi cha Azam FC ilikuwa ya mchezaji muhimu wa mzunguko 'rotation player', lakini hakuwa chaguo la kwanza chini ya kocha Florent Ibenge, jambo ambalo linawapasua kichwa mashabiki wa Simba wakiamini atashindwa pia kuwika akiwa na timu yao.


SIKIA UPANDE WA CHILAMBO

Akizungumza na Mwanaspoti mmoja kati ya watu wa karibu wa beki huyo alisema, Azam ndiyo iliyomzingua Chilambo kwani ilishamwambia itamuita mezani lakini haikufanya hivyo na mwenyewe anaona muda unazidi kwenda.

"Chilambo ameamua kuondoka kwa sababu ameona Azam haina mpango wa kumuita kwani anaona muda unaenda hivyo akaamua kufanya uamuzi wake wa haraka kwani ligi iko mwishoni.

"Azam ni kama haimtaki kwani ingekuwa inania naye basi wangeshafikia makubaliano, ndio maana ameamua kwenda kwenye timu ambayo inamtaka na kukaa nao mezani kufanya mazungumzo ya mapema."

Chilambo alipata umaarufu akichezea Ruvu Shooting msimu wa 2021/2022, alikuwa nguzo muhimu ya timu hiyo akionyesha uwezo mkubwa wa kuzuia na kushambulia kutokea pembeni, kiwango kilichowavutia mabosi wa Azam na kumsajili.


MECHI ZILIZOSALIA AZAM

Juni 12, 2026: Fountain Gate FC dhidi ya Azam FC (Ugenini).

Juni 16, 2026: Azam FC dhidi ya Mashujaa FC (Nyumbani).

Juni 24, 2026: Yanga dhidi ya Azam FC (Ugenini).

Juni 27, 2026: Coastal Union dhidi ya Azam FC (Ugenini).

Juni 30, 2026: Azam FC dhidi ya Dodoma Jiji FC (Nyumbani).