Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BDL ilihamia Taifa Cup

BDL Pict

Muktasari:

  • Mara iliwakilishwa na mastaa kama Baraka Sabibi, Mussa Chacha wanaokipiga JKT ilhali Abass Omary, Mwinyi Pembe, Jonas Mushi, Evance Davies na Tyrone Edward wanaichezea Stein Warriors.

Ushindani wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), ulihamia katika fainali ya mashindano ya Kombe la Taifa kati ya Dar es Salaam na Mara, ambapo ulitokana na ubora wachezaji wa timu zote mbili kutokana na jinsi walivyozoeana wakutanapo kwenye BDL.

Mara iliwakilishwa na mastaa kama Baraka Sabibi, Mussa Chacha wanaokipiga JKT ilhali Abass Omary, Mwinyi Pembe, Jonas Mushi, Evance Davies na Tyrone Edward wanaichezea Stein Warriors.

Nayo Dar es Salaam iliwakilishwa na Amin Mkosa pamoja Haji Mbegu wanaocheza Dar City, Elias Nshishi na Alinani Msongole wapo ABC, Jimmy Brown na Omary Ndula wanakipiga JKT huku Josephat Peter anaichezea Pazi.