Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baresi: Wakitua hawa tu, mmekwisha

Bares Pict

Muktasari:

  • Kocha Abdallah Mohamed ‘Baresi’ amesema kwa aina ya kikosi alichonacho, ana mpango wa kuongeza wachezaji wachache kulingana na upungufu uliopo, kubwa zaidi akitaka kiungo mkabaji na mshambuliaji ambao anaamini wataifanya Mashujaa iwe na moto zaidi ya iliyoanza nayo mwanzoni mwa msimu huu.

MASHUJAA jana ilipoteza kwa mabao 3-1 mbele ya Dodoma Jiji ikiwa ni kipigo cha tano kwa timu hiyo katika mechi 16 za Ligi Kuu Bara ilizocheza hadi sasa, lakini kocha wa timu hiyo amesema wanaenda mapumziko kujipanga upya na kubwa anachofanya ni kuongeza mashine chache kikosini ili mambo yawe matamu zaidi.

Kocha Abdallah Mohamed ‘Baresi’ amesema kwa aina ya kikosi alichonacho, ana mpango wa kuongeza wachezaji wachache kulingana na upungufu uliopo, kubwa zaidi akitaka kiungo mkabaji na mshambuliaji ambao anaamini wataifanya Mashujaa iwe na moto zaidi ya iliyoanza nayo mwanzoni mwa msimu huu.

Kipigo cha juzi usiku kilichopatikana kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kimeifanya Mashujaa kusalia na pointi 19 baada ya mechi 16, ikishinda nne na kutoka sare saba huyo ikipoteza mara tano na Baresi alisema amekubali wameteleza, lakini anaenda kuimarisha kikosi ili warudi Januari 2025 na moto.

Akizungumza na Mwanaspoti, Baresi alisema hahitaji kuongeza wachezaji wengi katika dirisha hili kutokana na timu yake kuwa imara maeneo mengi huku akiweka wazi kuwa wanamkosa mchezaji ambaye anaweza kuwalisha washambuliaji wake pamoja na kiungo mkabaji ili kupunguza makosa eneo la ulinzi.

“Hatupo vibaya sana tuna timu imara na ya ushindani shida ni maeneo hao mawili naamini tukimpata kiungo mmoja wa ushambuliaji ambaye atafanya kazi kwa usahihi akisaidiana na washambuliaji waliopo Emmanuel Mtumbuka aliyekuwa nje kwa muda akiuguza majeraha na Crispin Ngushi tutaweza kufikia malengo,” alisema Baresi.