Barca yailima Real Madrid 3-0 ikitangulia fainali Kombe la Copa del Rey

Muktasari:
- Mabao ya Barcelona yalifungwa na Luis Suarez dakika za 50 na 73, huku Raphael Verane akitupia bao moja dakika ya 69.
Nyota Luis Suarez ameitibulia Real Madrid kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu baada ya kufunga mabao mawili na kuipelea timu yake kwenye fainali ya Copa del Rey.
Suarez alipelekea mauaji hayo akifunga bao la tatu kwa mkwaju wa penalti na kuitupa nje Real Madrid kwenye mashindano hayo.

Kabla ya mchezo huo wa ambao ilikuwa ni fainali ya pili, awali timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 kwenye nusu fainali ya kwanza iliyopigwa hivi karibuni.

Mabao ya Barcelona yalifungwa na Luis Suarez dakika za 50 na 73, huku Raphael Verane akitupia bao moja dakika ya 69.

Wachezaji wawili wa Bracelona Segio Busquets na Nelson Semedo walilimwa kadi za njanoPia upande wa Real Madrid wachezaji wao Lucas Vazquez na Casemitro walilimwa kadi za njano.

Hivyo, Barcelona imetinga hatua ya fainali baada ya kuvuka kwa jumla ya mabao 4-1.
