Bandari yaifungasha virago Singida United ikiifunga bao 1-0

Muktasari:

Licha ya Singida United kupoteza 1-0, dhidi ya Bandari FC wao ndio walikuwa wakicheza na kutawala mpira.

Timu ya Bandari ya Kenya imeiondoa Singida United kwenye mashindano ya SportPesa Cup baada ya kuifunga bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo Jumanne.
Dakika 49 Singida walifanya mabadiliko katika eneo la ushambuliaji baada ya kumtoa Awesu Awesu na kuingia Benedict Beda ili kuongeza nguvu katika eneo hilo.
Singida United walifanya mabadiliko mengine kwa kumtoa Salum Kipanga na kuingia Jonathan Daka ambaye alienda kuongeza nguvu katika nafasi ya ulinzi.
Mabadiliko katika upande wa ushambuliaji ya Singida ulionyesha kujibu baada ya kombinesheni nzuri ya Maganga ambaye alikuwa anaongezeka kusaidiana na Benedict Beda, ambapo dakika 55 Maganga alipiga shuti kali na kugonga mwamba .
Bandari walifanya shambulizi la haraka dakika 59 baada ya William Wadri kuoiga pasi ya mwisho kwa Darius Msagha ambaye aliingia na mpira ndani ya boksi hata hivyo alipiga nje, wakati huo huo wakafanya mabadiliko ya kumtoa Msagha na kuingia Taro Leonard.
Dakika 66 Bandari walipata penalti iliyopigwa na William Wadri na kuianfikia Bandari goli la kuongiza, baada Boniphace Maganga kuunawa mpira uliopigwa na Taro Donald ndani ya boksi.
Goli hilo halikuwafanya singida washindwe kushambulia kwani walionekana kujipanga na kuzidisha mashambulizi.
Dakika 77 Yusuh Kagoma wa Singida alikosa goli akiwa ndani ya boksi baada ya kuwapiga chenga mabeki wa Bandari hata hivyo shuti lake lilienda nje.
Singida walifanya mabadiliko dakika 81 kwa kumtoa Frank Zakaria na kuingia Habib Kyombo ambaye ndio mshambuliaji wao tegemeo katika kikosi hiko.
Kwa matokeo haya kunaifanya Singida kutolewa katika mashindano haya.

MCHEZO ULIVYOKUWA
Licha ya singida kupoteza 1-0 dhidi ya Bandari wao ndio walikuwa wakicheza na kutawala mpira.
Hata hivyo upande wa Bandari wao walikuwa wkaifana mashambulizi ya kushtukiza na mojawapo ndio liliwapatia bao.
Kitendo cha singida kumuanzisha nje mshambuliaji wao, Habib Kyombo kulionekana kuwaumbua kwani mshambuliaji huyo alivyoingia alionyesha uhai katika safu hiyo ya ushambuliaji.