Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bajana aongeza mzuka Azam FC

Muktasari:

  • Bajana alipata majeraha Desemba 11, 2023 kwenye Uwanja wa Azam Complex katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao Azam FC ilishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Maafande wa JKT Tanzania na kumfanya kukosekana kwa muda mrefu kikosini humo.

BAADA ya kukaa nje kwa muda wa takribani miezi 10, nahodha na kiungo wa Azam FC, Sospeter Bajana ameanza mazoezi mepesi katika kikosi hicho na wakati wowote kuanzia sasa atajiunga na wenzake kwa ajili ya kucheza michezo mbalimbali msimu huu.

Bajana amekuwa nje ya uwanja tangu Desemba 11, mwaka jana baada ya kupata majeraha ya mifupa ya nyonga ya kulia na ya kushoto (pubis symphysis), yaliyomfanya Mei mwaka huu kupelekwa Afrika Kusini katika Hospitali ya Life Vincent Pallotti jijini Cape Town.

Akizungumza na Mwanaspoti jijini Dar es Salaam, Daktari wa Azam FC, Mbaruku Mlinga amesema kwa sasa Bajana amekabidhiwa kwa kocha wa utimamu wa mwili, Ouajou Driss kwa ajili ya kurejesha ufiti wake na muda sio mrefu atajumuika na wenzake.

“Tayari ameshaondoka katika mikono yetu kwa maana ya idara ya tiba kwa wanamichezo, upasuaji wake ulikuwa mkubwa hivyo, kabla ya kuuungana rasmi na wenzake inabidi apitie kwa kocha wa utimamu wa mwili ili aendelee kuangalia maendeleo yake,” amesema.

Mlinga aliongeza, hali ya kikosi hicho kwa sasa ni nzuri na kipa, Mohamed Mustafa aliyepata majeraja akiwa na timu yake ya taifa ya Sudan, anaendelea vizuri na muda wowote kuanzia sasa atajiunga na wachezaji wenzake kwa ajili ya kucheza.

“Majeraha yake hayakuwa makubwa sana na licha ya kukosa michezo mitatu ya Ligi Kuu Bara ila kwa sasa yupo fiti asilimia 100 na muda wowote ataanza kuonekana uwanja akicheza, hali ya nyota wengine ni nzuri hivyo kilichobaki ni kwa benchi la ufundi,” amesema.

Bajana alipata majeraha Desemba 11, 2023 kwenye Uwanja wa Azam Complex katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao Azam FC ilishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Maafande wa JKT Tanzania na kumfanya kukosekana kwa muda mrefu kikosini humo.