Bahati Mgunda apeleka ujuzi Namibia

Muktasari:
- Mgunda alichaguliwa na Fiba Afrika kuwa mkufunzi kutokana na mafunzo ya siku tano yaliyofanyika nchini yalishirikisha watoto 85 na kuchaguliwa kuwa kiongozi wa makocha kutoka Afrika.
KOCHA mkongwe wa mpira wa kikapu, Bahati Mgunda ni miongoni mwa makocha 17 wanaotarajiwa kutoa mafunzo kwa watoto nchini Namibia, yalijulikanayo kama Min Basketball yatakayofanyika Uwanja wa Shule ya Augustinium.
Mgunda alichaguliwa na Fiba Afrika kuwa mkufunzi kutokana na mafunzo ya siku tano yaliyofanyika nchini yalishirikisha watoto 85 na kuchaguliwa kuwa kiongozi wa makocha kutoka Afrika.
Alisema wakati wa mafunzo hayo, alitambulisha pia mchezo wa wheelchair basketball na anatarajia kurudi Namibia siku zijazo kutokana na mwaliko wa chama cha mpira wa kikapu cha nchi hiyo.
“Nitakwenda kutoa mafunzo zaidi kwa makocha, ikiwamo kusaidia katika kuweka mfumo sahihi wa elimu na makocha.
“Jambo ambalo nina uzoefu nalo kupitia chama cha makocha wa mpira wa kikapu Tanzania, ni pamoja na kushiriki kuandaa programu ya elimu na makocha kupitia TBF,” aliongeza Mgunda.
Mafunzo hayo yalienda sambamba na mafunzo yajulikanayo Region 5 youth games ya umri wa miaka 16, yaliyoshirikisha nchi zilizoko Kusini mwa Afrika.