Azam yawapa kikosi kilichomuua Fasil Kenema kuivaa KMC

Muktasari:
Katika mchezo huo kocha wa Azam, Ettiene Ndayiragije amekianzisha kikosi kilekile ambacho kilianza katika mchezo wao wa pili dhidi ya Fasil Kenema.
Dar es Salaam. Kocha wa Azam, Ettiene Ndayiragije amekianzisha kikosi kilekile kilichopata ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Fasil Kenema leo wanaposhuka uwanjani kuivaa KMC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Mabingwa hao wa Kombe la FA, Azam wamefanikiwa kufuzu kwa hatua ya kwanza wa Kombe la Shirikisho barani Afrika, kwa kuitoa klabu ya Kenema kwa jumla ya mabao 3-2, hivyo wataingia uwanjani kuivaa KMC kwa lengo la kuendeleza rekodi yao ya ushindi.
Mchezo huu unatarajia kuwa mkali kwa timu zote, huku KMC wakiwa na machungu baada ya kuondolewa na As Kigali katika kombe la Shirikisho baada ya kufungwa 1-2.
Kikosi Azam kinachocheza dhidi ya Kmc , Razack Abarola, Nickolas Wadada, Bruce Kangwa, Yakub Mohammed, Daniel Amoah, Frank Domayo, Emmanuel Mvuyekure, Salum Abubakar, Richard Djodi, Obrey Chirwa na Idd Seleman.
Kwa upande wa wachezaji wa akiba, Mwadini Ally, Oscar Masai, Salmin Hoza, Masoud Abdallah, Idd Kipagwile, Donald Ngoma na Paul Peter.
Kikosi hiki akijabadilika chochote kuanzia wachezaji waliocheza mpaka wale waliokuwa wamekaa katika benchi.