Azam wataja kinachowabeba

Friday October 09 2020
azam pic

OFISA Mtendaji mkuu wa klabu ya Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesema siri kubwa ya wao kuanza vizuri msimu huu imetokana na utlivu wakati wa usajili.

Azam mpaka sasa ndio inaoongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 15 katika mechi tano ilizocheza huku ikiruhusu magoli mawili na kufunga magoli tisa na haijapoteza wala kutoka sare mchezo wowote.

Popat alisema hakuna siri kubwa iliyopo zaidi ya usajili wa maana ambao imeufanya na ndio unaowafanya timu yao ionekane kuwa bora msimu huu.

“Motisha tu na usajili mzuri wa kiuweledi, hatujakurupuka kusajili, motisha tunawapa lakini ni ya kawaida” alisema Popat kwa kifupi huku akiwapongeza vijana wake.

 

Advertisement