Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam, Pyramid ngoma ngumu

Muktasari:

SULUHU iliyopata Azam FC katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Pryamid ya Kombe la Shirikisho Africa, inawapa kazi ya ziada ya kufanya ugenini.

SULUHU iliyopata Azam FC katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Pryamid ya Kombe la Shirikisho Africa, inawapa kazi ya ziada ya kufanya ugenini.

Katika kipindi cha kwanza Azam walikuwa wanatengeneza nafasi lakini hawakuweza kuingiza mpira wavunii

Katika kipindi cha pili timu zote ziliingia kwa spidi na kuonyesha wanahitaji bao la kuongoza katika mchezo huo.

Azam walitoka katika mfumo wa 4-5-1 na kucheza 4-4-2 ambayo winga Idd Nado alikuwa anaongezeka mbele kusaidiana na Idris Mbombo.

Licha ya Nado kuongezeka bado umakini ulikuwa mdogo kwa washambuliaji wa Azam kuhakikisha wanapata mabao.

Dakika 48 Idd Nado wa Azam alionyeshewa kadi ya njano baada ya kumkanyaga kwa nyuma kiungo wa Pyramid, Nabil Aly.

Dakika 58 Pyramid walifanya mabadiliko wakimtoa Mahmoudy Wady ambaye aliumia na kuingia Mohamed Elgabbas.

Dakika 60 Pyramid walitaka kupata bao kupitia kwa Ibrahim Hassan ambaye aliwapangua mabeki wa Azam na kufyatuka shuti ambalo lilipanguliwa na kipa Mathias Kigonya na kuwa kona isiyokuwa na faida.

Wakati huo huo Azam walifanya mabadiliko ya kuingia Ismail Aziz na kutoka Charles Zulu, mabadiliko hayo yalikuwa ni kwenda kuongeza nguvu eneo la ushambuliji akitokea pembeni.

Dakika 69 kiungo wa Azam, Paul Katema alionyeshewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Ibrahim Hassan.