Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam inavyotembea na Simba

Simba Pict
Simba Pict

Muktasari:

  • Awali Simba ndio waliokuwa vinara wa kukusanya pointi nyingi nyumbani ambapo ndani ya michezo sita waliyocheza katika ligi, vijana hao wa Fadlu Davids walizifunga KMC (4-0), Namungo (3-0), Fountain Gate (4-0), Tabora United (3-0), wakapoteza dhidi ya Yanga (1-0) na toa sare dhidi Coastal Union (2-2) ya Tanga.

USHINDI wa mabao 2-1 ambao Azam FC iliupata juzi ikiwa Azam Complex dhidi ya Singida Black Stars, umewafanya matajiri hao wa Chamazi kuifikia Simba kwa kukusanya pointi nyingi zaidi (13) katika mechi za nyumbani Ligi Kuu Bara msimu huu.

Awali Simba ndio waliokuwa vinara wa kukusanya pointi nyingi nyumbani ambapo ndani ya michezo sita waliyocheza katika ligi, vijana hao wa Fadlu Davids walizifunga KMC (4-0), Namungo (3-0), Fountain Gate (4-0), Tabora United (3-0), wakapoteza dhidi ya Yanga (1-0) na toa sare dhidi Coastal Union (2-2) ya Tanga.

Kwa upande wa Azam FC, wenyewe wamekusanya pointi hizo kwa kuzifunga Singida Big Stars (2-1), Kagera Sugar (1-0), Kengold (4-1), Coastal Union (1-0), wamepoteza dhidi ya Simba (2-0) na kutoa suluhu dhidi ya Pamba Jiji ya Mwanza.

Katika michezo hiyo sita ya nyumbani, Simba ndio vinara wa mabao kwa kupachika 16 huku wakiruhusu mabao matatu, Azam wamefunga mabao manane na kuruhusu manne, mbali na Simba na Azam timu nyingine ambazo zimevuna pointi nyingi nyumbani ni Dodoma Jiji imevuna pointi 12 katika michezo mitano, imeshinda mechi nne na kupoteza moja.

Maafande wa JKT Tanzania wanashika nafasi ya nne kwa kukusanya 11 pointi ndani ya mechi tano, wameshinda tatu na kutoa sare mbili na ndio timu pekee katika ligi msimu huu ambayo haijapoteza katika uwanja wake wa nyumbani.

Katika orodha ya timu ambazo zimekusanya pointi nyingi nyumbani, Yanga inashika nafasi ya 10, ndani ya mechi tano wameshinda tatu dhidi ya JKT Tanzania (2-0), Pamba Jiji (4-0) na KMC (1-0) na kupoteza mbili dhidi ya Azam FC kwa bao 1-0 na Tabora United kwa mabao 3-1 hivyo wamevuna pointi tisa.

Pamba Jiji ndio wanaburuza mkia wakiwa hawajashinda mchezo hata mmoja wakiwa nyumbani, wamevuna pointi nne kwa kutoa sare na kupoteza michezo miwili.

Akizungumzia mwenendo wa kikosi chake baada ya ushindi wa nane msimu huu katika ligi huku wakifikisha pointi 27 nyuma kwa pointi moja waliyoachwa na Simba, kocha wa Azam FC, Rachid Taoussi aliwapongeza wachezaji wake kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya dhidi ya Singida Black Stars.

“Haukuwa mchezo mwepesi, tulihitaji pointi tatu ili kuendelea kupunguza utofauti wa pointi baina yetu na Simba, bado tunakazi kubwa ya kufanya mbele yetu,” alisema kocha huyo.

Katika mchezo huo, mabao ya Azam yalifungwa na Feisal Salum ‘Feitoto’ na Jhonier Blanco huku la kufutia machozi la Singida Big Stars likifungwa na Elvis Rupia ambaye lilikuwa bao lake la tano msimu huu katika Ligi Kuu Bara.

Azam FC imecheza mechi 12, huku Simba ikiwa nazo 11 katika mashindano hayo.