Aucho, Bangala jeuri ya Nabi

Thursday September 30 2021
AUCHO PIC
By Khatimu Naheka

YANGA jana walikuwa wakimalizana na Kagera Sugar katika pambano la kwanza la Ligi Kuu Bara msimu huu, huku kocha mkuu, Nasreddine Nabi akitamba ubora wa viungo Khalid Aucho na Yannick Bangala unavyompa mzuka kikosini kwa sasa.

Viungo hao walicheza pamoja katika Ngao ya Jamii dhidi ya Simba na kuelewana sana wakiilinda beki na Kocha Nabi alisema anaamini wataendelea kuwa bora zaidi, lakini hatua kubwa yao itamsaidia nahodha msaidizi, Mukoko Tonombe kuwa bora zaidi.

“Wanacheza vizuri, lakini bado kuna ubora zaidi utaongezeka kama wataendelea kujituma. Walionyesha ni wachezaji wenye uzoefu mkubwa ambao watasaidia timu,” alisema Nabi.

“Ubora wao utaongeza ushindani kwa wengine, msimu uliopita tulimtumia zaidi Mukoko, alifanya kazi nzuri. Siku zote nimekuwa naamini katika ubora wa mchezaji kupitia ushindani..”

Advertisement