Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arajiga, Sasii ndo hivyo tena huko

LICHA ya baadhi ya waamuzi kumaliza adhabu zao za kufungiwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Nassor Hamduni amesema wataendelea kuwa chini ya uangalizi maalumu hadi pale watakapojiridhisha.

Hamduni alikiri kuwepo kwa waamuzi ambao wamemaliza adhabu walizopewa lakini amesisitiza kwa sasa kuwaweka kwenye ratiba ni mapema hadi pale watakapoona inafaa kuwarejesha.

Mmoja ya waamuzi ambao wamemaliza adhabu ni pamoja na Ahmed Arajiga ambaye alifungiwa miezi sita kutokana na makosa mbalimbali ya kujirudia katika kutafsiri sheria za soka uwanjani.

“Bado hatujawarejesha hadi sasa ili tuone namna gani tutafanya hivyo, wanaweza wakarejea uwanjani kama ambavyo nia yetu ilivyo lakini wanaweza wakaonekana msimu ujao.

“Kwa sasa siwezi kufanya tathmini ya kiwango cha waamuzi kama kimeongezeka au kimepungua lakini msimu ukimalizika naweza kufanya hivyo kwa kuangalia ripoti mbalimbali,” alisema Hamduni.

Hata hivyo, aliongeza kuna baadhi wamesharudishwa ndio maana kunaonekana kuna ubora katika michezo ya ligi mbalimbali zinazoendelea tofauti na hali ilivyokuwa siku za nyuma.

“Arajiga licha ya kumaliza miezi sita lakini yupo katika uangalizi kama ilivyo kwa kina, Sasii (Elly) na wengine, hivyo tunaomba wadau watuvumilie kidogo,” alisema.

Hamduni alisema anashukuru ligi hadi sasa inaendelea vyema na matumaini itamaliza salama kwa waamuzi kuchezesha kwa kufuata haki.