Arafat: Simba, Yanga ziache kusaidia wageni

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima Zanzibar (ZIC), Arafat Haji

MAKAMU wa rais wa Yanga, Arafat Haji amesema Simba na Yanga zina nafasi ya kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa ikiwa zinatajipanga vizuri na kutumia zaidi uwanja wa nyumbani na mashabiki wakiacha kusaidia wageni.

Arafat ambaye alikuwa akichangia mjadala kwenye Mwananchi X Space leo amesema Simba na Yanga zinaweza kupita licha ya kuingia kwenye hatua hiyo kama timu zisizopewa nafasi kubwa ya kusonga mbele.

"Uwezekano wa kufika mbali upo na ni mkubwa sana lakini huwezi kufika hapo bila yakuwa na mipango ya muda mfupi na mrefu."

"Berkane na Algers hizi ni timu ambazo zilikuwa na mipango ambayo inabadilika kulingana na hatua.

Hivi ndivyo sisi Yanga tunavyokwenda, tulikuwa na mipango ya awali ya kufika hatua ya makundi, hiyo ilikuwa ni mpango wa muda mfupi lakini tumefanikiwa kufuzu na sasa tupo robo.

Hayo yamesemwa leo Machi 13, 2024 kwenye mjadala wa Mwananchi X Space ulioandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd wenye mada isemayo; Ipi nafasi ya Simba, Yanga kwenye vita ya kusaka nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.