Amir Maftah aeleza alivyotaabika kucheza soka Msumbiji
Muktasari:
Maftah aliachwa Yanga mwaka 2010 na kutimkia kwa watani zao wa jadi Simba kabla ya kwenda Msumbiji
Dar es Salaam.Beki wa zamani wa Yanga, Simba na Kagera Sugar, Amir Maftah amesema alipata wakati mgumu kuzoea maisha ya soka ya Msumbiji.
Maftah anayechezea klabu ya 3 de Fevereiro de Quelimane ya Ligi daraja la kwanza au Segunda amesema uvumilivu ndiyo umemsaidia.
Maftah sasa ametimiza miaka miwili akicheza soka la kulipwa Msumbiji amesema licha ya kupewa ushirikiano na wenyeji, lugha ya Kireno ilimsumbua.
"Nilipata tabu mno kuzoea mazingira, lugha na asili ya huku, lakini nilivumilia na polepole nimeanza kuzoea," alisema mchezaji huyo.
Alisema Msumbiji wana tamaduni za kizungu zaidi kulinganisha na Tanzania ambako aliishi na kuzoea miiko na tamaduni za kiafrika.