Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Allarakhia atambulishwa Boreham

RAKIA PICTR

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa Flashscore, thamani ya kiungo mshambuliaji huyo imepanda baada ya uhamisho wake kutoka Rochdale ambako aliitumikia msimu mmoja alipokuwa na kiwango bora kwenda Boreham.

KAMA kuna Mtanzania anayevuna matunda ya kazi yake kimyakimya kupitia soka, basi miongoni mwao ni kiungo wa Taifa Stars, Tarryn Allarakhia, ambaye amejiunga na klabu ya Boreham Wood ya England huku thamani yake ya soko ikipaa kutoka Sh150 milioni mwaka 2024 hadi kufikia zaidi ya Sh10 bilioni.

Kwa mujibu wa Flashscore, thamani ya kiungo mshambuliaji huyo imepanda baada ya uhamisho wake kutoka Rochdale ambako aliitumikia msimu mmoja alipokuwa na kiwango bora kwenda Boreham.

Kupaa kwa thamani yake kunachangiwa na kiwango bora alichokionyesha katika ngazi ya klabu na timu ya taifa, hali iliyomfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wa Tanzania wanaovutia zaidi katika soko la usajili.

Pia, kitendo cha kuitwa mara kwa mara kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars ni mojawapo ya sababu ya thamani yake kuongezeka.

Kwa England, hata kama mchezaji anacheza ligi ndogo anapoitwa timu ya Taifa thamani yake inaongezeka, hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Allarakhia ambaye ana asili ya Tanzania.

Allarakhia mwenye umri wa miaka 28, ametua Boreham Wood inayoshiriki National League baada ya kuachwa na Rochdale mwishoni mwa msimu uliopita.

Kiungo huyo alianza safari yake ya soka la kulipwa akiwa Colchester United, lakini hakupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kabla ya kuhamia Crawley Town mwaka 2018. Baadaye alizitumikia Wealdstone na Woking kabla ya kutua Rochdale mwaka 2024.

Akiwa Rochdale alicheza mechi 75 katika mashindano yote. Msimu uliopita alicheza mechi 30 na kuwa sehemu muhimu ya kikosi hicho kilichofanikisha kurejea English Football League baada ya kupanda daraja.