Aliyeiua Stars atua Yanga

Monday October 12 2020
said pic

Yanga imemsainisha mkataba wa miaka mwili mshambuliaji Said Ntibazonkiza baada ya kung'aa zaidi katika mchezo w Taifa Stars dhidi ya Burundi.

Mshambuliaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili ambapo atatua haraka nchini kuja kuanza kuitumikia klabu hiyo mara baada ya dirisha dogo kufunguliwa.

Ntibazonkiza ndiye aliyeipa Burundi bao pekee la ushindi wa 1-0 dhidi ya Taifa Stars kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kalenda ya Fifa uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Hatua ya Yanga kuinasa saini ya mshambuliaji huyo imekuwa rahisi baada ya kumaliza mkataba na klabu yake ikiwa ni hesabu za muda mrefu.

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM Mhandisi Hersi Said amesema hesabu zao katika kumuwinda mshambuliaji huyo zilikuwa za muda mrefu lakini walishindwa kukamilisha awali katika dirisha lililopita kufuatia klabu yake kuweka ngumu kumuachia.

"Alikuwa na mkataba na klabu yake tukazungumza nao lakini hawakutaka kumuachia na muda haukuwa rafiki lakini sasa ameumaliza mkataba na yuko huru," amesema Hersi.

Advertisement

"Amesaini mkataba wa miaka miwili utakaoanza sasa na tumeshamalizana naye kila kitu nafikiri atajiunga na timu sio muda mrefu.

Advertisement