Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ali Kamwe aaga Jangwani, ataja sababu

Muktasari:

  • Kamwe aliyehudumu katika nafasi hiyo kwa miaka miwili amethibitisha kuondoka Yanga kupitia ukurasa wake wa mtandao w Instagram leo Jumapili Julai 28, 2024.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe ametangaza kuachia nafasi hiyo huku akisema muda wake umemalizika.

Kamwe aliyehudumu katika nafasi hiyo kwa miaka miwili amethibitisha kuondoka Yanga kupitia ukurasa wake wa mtandao w Instagram leo Jumapili Julai 28, 2024.

"Mtumbuizaji mzuri anatakiwa kujua ni wakati gani wa kuondoka Jukwaani. Maneno ya hekima kutoka katika kinywa cha Patrick Loch Otieno Lumumba.

"Na ni Hekima hii, inanituma mbele yenu Wananchi, mashabiki na wanachama wa Klabu yetu pendwa, kuwaambia kuwa, Ni wakati sasa wa kijana wenu kuondoka Jukwaani," ameandika Kamwe.

Kamwe ameongeza kuwa muda wake umemalizika na anawashukuru sana.

Endelea kufuatilia Mwanaspoti kwa taarifa zaidi