Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Al Ahly Benghazi yatua kwa Paul Peter

BENGHAZI Pict

Muktasari:

  • Peter mwenye miaka 27, amemaliza msimu akiwa na mabao tisa, asisti tatu na alikuwa na kiwango cha juu. Huo ni muendelezo wa kiwango alichokionyesha katika misimu miwili aliyokuwa Dodoma Jiji akifunga mabao 11.

KUNA taarifa za mshambuliaji wa JKT Tanzania, Paul Peter kuhitajika na klabu ya Al Ahly Benghazi, ili kumsajili kwa ajili ya msimu ujao, baada ya kufanya vizuri msimu uliomalizika.

Chanzo kutoka Libya kilisema, timu hiyo imepeleka ofa kwa uongozi wa nyota huyo, ambao bado wanaichambua kama inaweza ikawa na manufaa kwa mchezaji huyo, licha ya kuwa fursa kwenda kupata chalenji mpya nje lakini wanaweka mbele maslahi.

BENGH 01

Peter mwenye miaka 27, amemaliza msimu akiwa na mabao tisa, asisti tatu na alikuwa na kiwango cha juu. Huo ni muendelezo wa kiwango alichokionyesha katika misimu miwili aliyokuwa Dodoma Jiji akifunga mabao 11.

Chanzo kutoka Libya kilisema: “Kuna mawakala ambao wanafuatilia wachezaji kutoka nchini mbalimbali ikiwemo Tanzania ambayo kwa sasa soka lake lipo juu, miongoni mwa hao ni Peter ambaye kiwango chake kimekuwa kikubwa.”

BENGH 02

Alipotafutwa mchezaji huyo ili kuthibitisha kinachoendelea kuhusishwa na Al Ahly Benghazi, amesema: “Natambua kuna ofa kama nilivyoambiwa na meneja wangu, lakini bado hatujakaa na kuzungumza kwani ndiyo kwanza tumetoka kumaliza msimu wa Ligi Kuu Bara.