Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AKILI ZA KIJIWENI: JKT Queens ikimshusha Simba Queens sijui

JKT Pict

Muktasari:

  • JKT Queens ilikuwa mbele kwa tofauti ya pointi moja tu dhidi ya Simba Queens ambayo ilikuwa nafasi ya pili na pointi zake 37, timu zote zikiwa zimecheza idadi sawa ya mechi ambayo ni 14.

KABLA ya mechi ya mechi ya jana ya Ligi Kuu ya Wanawake ambayo JKT Queens ilikuwa nyumbani dhidi ya Simba Queens, maafande hao walikuwa wanaongoza msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 38.

JKT Queens ilikuwa mbele kwa tofauti ya pointi moja tu dhidi ya Simba Queens ambayo ilikuwa nafasi ya pili na pointi zake 37, timu zote zikiwa zimecheza idadi sawa ya mechi ambayo ni 14.

Sasa jana miamba hiyo miwili ya soka la wanawake ikakutana, huku JKT Tanzania ikiwa mwenyeji kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam katika mchezo ambao ungetoa taswira ya ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.

Kimahesabu, JKT Queens walikuwa na faida mbili kabla ya mechi hiyo ambazo ya kwanza ni pengo la pointi moja hivyo hata wangetoka sare, bado msimamo wa ligi ungewaweka nafasi kubwa ya kutwaa taji.

Lakini faida nyingine ilikuwa ni kucheza katika uwanja wake wa nyumbani hivyo ingenufaika na uwepo wa mashabiki na yenyewe imeuzoea vizuri kuliko wageni wao Simba Queens.

Simba Queens haikuwa na lingine lolote ambalo lingeisaidia baada ya mchezo huo tofauti na ushindi kwani kwa kufungwa au kutoka sare maana yake JKT Queens ingeendelea kukaa kileleni na wao matumaini ya ubingwa yangepotea.

Hata hivyo, Simba Queens ikaenda Meja Jenerali Isamuhyo kwa shauku kubwa ya kuvuna pointi tatu na ikafanya hivyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 matokeo ambayo yameipeleka kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake ikifikisha pointi 40.

Kitendo cha Simba Queens kukaa kileleni baada ya ushindi wa jana ni wazi kimeiweka kwenye wakati mgumu JKT Queens kuwashusha na kutwaa taji maana kila timu imebakisha mechi tatu tu ili iweze kumalizia msimu ukizubaa tu imekula kwako.

Na kwa namna Simba Queens ilivyopitia kipindi kigumu msimu huu hadi ikafanikiwa kurudi tena kileleni, haiwezi kuwa rahisi kukubali kumpisha tena JKT Queens pale juu na kiufupi ni kama imeisha hiyoooo.