Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ajibu, Mussa wamponza Mayanga

Muktasari:

Mussa anayeichezea Ruvu Shooting alimaliza msimu uliopita akiwa na mabao 14 huku Ajibu aliyepo Yanga kwa sasa alikuwa na mabao manane akiichezea Simba na kuisaidia kuiweka kwenye mbio za ubingwa, lakini wote wameachwa kwenye kikosi cha timu hiyo na kusababisha lawama kwa Kocha Mayanga kuwa anawabania tu.

TAIFA Stars chini ya Kocha Salum Mayanga, imeonekana kuwa na tatizo katika safu yake ya ushambuliaji, lakini kitu cha ajabu nje ya kikosi hicho kuna mastraika tishio kwa kucheka na nyavu, Ibrahim Ajibu na Abdulrahman Mussa.

Mussa anayeichezea Ruvu Shooting alimaliza msimu uliopita akiwa na mabao 14 huku Ajibu aliyepo Yanga kwa sasa alikuwa na mabao manane akiichezea Simba na kuisaidia kuiweka kwenye mbio za ubingwa, lakini wote wameachwa kwenye kikosi cha timu hiyo na kusababisha lawama kwa Kocha Mayanga kuwa anawabania tu.

Mayanga ambaye wikiendi hii atakuwa na mtihani wa kurudiana na Rwanda mjini Kigali baada ya sare ya 1-1 ya CCM Kirumba jijini Mwanza katika mechi ya kuwania fainali za Chan 2018, ameshambuliwa na wadau kwa kuwaacha nyota hao.

Hata hivyo kocha huyo amefichua kuwa, Stars inahitaji matokeo mazuri na si majina ya wachezaji hivyo kwake kuwaita ama kutokuwaita Ajibu na Mussa haipaswi kuwa mjadala.

Mayanga aliliambia Mwanaspoti kuwa, wadau wa soka wanahitaji matokeo mazuri kutoka kwenye kikosi chake bila kujali nani ameifungia timu hiyo mabao, hivyo suala la Ajibu na Mussa ni jambo binafsi na hayapaswi kuingizwa kikosini.

“Mambo mengine ni ya kiufundi na yatabaki kuwa ya ufundi, Tanzania ina wachezaji wengi sana, ligi ina timu 16 zenye wachezaji wazuri hivyo sidhani kama Ajibu na Mussa ndiyo pekee ambao wangeweza kuipa matokeo mazuri Stars,” alisema kocha huyo.

“Naamini wadau wanahitaji matokeo mazuri na sio kuzungumzia mchezaji mmoja mmoja, hivyo nawaomba wadau jambo la msingi timu ipate matokeo na sio nani amecheza.”

Akizungumzia maandalizi ya mechi ijayo, alisema: “Tumeanza mazoezi leo (jana Jumatatu) asubuhi mpaka Ijumaa tunayafanyia kazi makosa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita maana lengo letu ni kusonga mbele kwenye michuano hii.

“Matokeo ya awali yamewapa taharuki kubwa mashabiki wetu, ni kweli ni jambo la kushtukiza ndiyo maana tunafanya kila jitihada kuhakikisha yale makosa ya awali hayatarudia.”

Stars ililazimisha sare ya kwa penalti la Himid Mao.