Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ajenda 11 kujadiliwa mkutano wa Simba

Ajenda 11 kujadiliwa mkutano wa Simba

Muktasari:

  • Ajenda 11 zitajadiliwa kwenye mkutano huo ikiwamo ya mapendekezo ya marekebisho ya kanuni za uchaguzi na katiba za klabu ya Simba.

Dar es Salaam. Hali ya utulivu imetawala wakati mchakato wa kuhakiki kadi za wanachama kwenye mkutano mkuu wa Simba ikiendea asubuhi hii kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.

Ajenda 11 zitajadiliwa kwenye mkutano huo ikiwamo ya mapendekezo ya marekebisho ya kanuni za uchaguzi na katiba za klabu ya Simba.

Mkutano huo uliochelewa kwa takribani saa moja ulitarajiwa kuanza majira ya saa 3:00 za asubuhi, huku wanachama wakiendelea kumiminika kushiriki mkutano huo.

Hadi kufikia saa 3:40 eneo la ukumbi wa chini ulikuwa umejaa huku watu wa itifaki wakitakiwa kuwaongoza wanachama wanaoendelea kuwasili ukumbini hapa kwenye viti vya eneo la juu la ukumbi huo.