Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yasaka rekodi mpya

Yanga yasaka rekodi mpya


Yanga imesaliwa na mechi nne ikiwamo ya Coastal Union, Polisi Tanzania, Mbeya City na Mtibwa Sugar ambako kama itatoka salama zote, itamfanya aiongoze timu hiyo kucheza mechi 37 bila kupoteza na kuifukuzia rekodi ya Azam iliyowekwa katika misimu mitatu mfululizo.

Nabi alisema anajua kuna mechi nne zilizosalia na anahitaji pointi tatu kubeba ubingwa, lakini kiu yake kufikia rekodi za Azam na Simba za kupoteza katika msimu mmoja na kuandika rekodi nyingine tamu kabla ya kuanza msimu mpya.

“Tumeanza maandalizi ya mechi zijazo kwa kufuata taratibu kwa wachezaji waliopo ukiachana na wale waliopo timu za taifa na tutaanzia gym kabla ya kuja uwanjani,” alisema Nabi na kuongeza;

“Lengo ya kufanya hivyo ni kuhakikisha wale wachezaji waliokuwa kwenye timu za taifa wakirejea kuungana na wenzao wote wawe sawa kiutimamu wa miili ili kwenda kushindana. Tunafanya yote hayo pamoja na ubora wa kikosi chetu kilivyo msimu huu tuweke rekodi yetu ya kutwaa ubingwa bila ya kupoteza mchezo kama ilivyokuwa wenzetu.”

Alisema mbali na kuwania rekodi hiyo katika Ligi, lakini anataka kuona wanashinda pia taji la ASFC dhidi ya Coastal Union aliokiri ni wazuri kwa mana walivyocheza na Azam na kuvuka hadi fainali.

Mara ya mwisho kwa Yanga kufungwa katika Ligi ilikuwa Aprili 25, mwaka jana waliponyukwa na Azam bao 1-0 la Prince Dube na kumaliza msimu huo ikicheza kucheza mechi saba baadae bila kupoteza na kuunganisha 26 za msimu huu, ikiwa kileleni na pointi 65, ikizidi Simba yenye 51.