Siri ya Wenger kutangaza kubwaga manyanga
Muktasari:
- Mabosi wa klabu wamewaza wakaona kuna tatizo, hakuna ubingwa wa Ligi Kuu, hakuna nafasi ya Ligi ya Mabingwa, itakwenda watakosa hata nafasi ya Ligi Europa na mwisho watakuwa wanabaki huko wanaowania kubakia Ligi Kuu.
London, England. Hakuna aliyetarajia kama kocha wa Arsenal, Arsenal wenger angetangaza kuachana na klabu mwisho wa msimu.
Mabosi wa klabu wamewaza wakaona kuna tatizo, hakuna ubingwa wa Ligi Kuu, hakuna nafasi ya Ligi ya Mabingwa, itakwenda watakosa hata nafasi ya Ligi Europa na mwisho watakuwa wanabaki huko wanaowania kubakia Ligi Kuu.
Wakaona wafanye kitu. Wakamwambia Wenger ajilipue kuwa mwisho wa msimu ataicha Arsenal.
Wenger alishtua dunia na kumbe kuna kilicho nyuma ya pazia. Mabosi wa klabu hawakutaka kumsikia Wenger akirudi msimu ujao na alisema pamoja na kukaa klabuni kwa miaka 22, tangazo alilolitoa si uamuzi wake.
Ijumaa iliyopita, Wenger 68, alitangaza kuwa ataachana na klabu mwishoni mwa msimu licha ya kuwa amebakisha mwaka mmoja kumaliza mkataba wake miaka miwili.
Kabla ya kukwaana na Atletico Madrid leo usiku, Wenger alisema: "Ninaangalia kile kilichopo mbele yangu. Kwa sasa ninafanya kazi kwa bidii mno.
Wenger akiamini anaweza kuivusha timu kwa hali yoyote, alisema hawezi kusema hatma lakini kila mmoja asubiri aone.
Kocha huyo alikuwa akijibu swali ya mwandishi wa habari wa Ujerumani alimtaka aeleze kwanini anaondoka wakati ana mechi muhimu zijazo.
"Kiukweli haukuwa uamuzi wangu, tulikutana na utawala na tukaelezana na baada ya makubaliano na ninafurahi kwamba ninaondoka na uamuzi wangu nimeutangaza katika wakati mwafaka," alisema.
Arsenal ilitwaa ubingwa mara tatu wa Ligi Kuu ya England, Kombe la FA mara saba, ikiwemo 1998 na 2002, chini ya Wenger.
Makocha wengi wanataka kibarua Arsenal akiwemo nahodha wa zamani wa timu hiyo, Patrick Vieira na kocha wa zamani wa Barcelona, Luis Enrique.
Kuhusu anadhani nani anaweza kuamrithi alisema: "Sitaki kushawishi wala kulazimisha, lakini kwa mtazamo ninadhani Luis Enrique."
Arsenal kupitia bosi wa timu, Ivan Gazidis alisema kuwa watatangaza kocha karuibuni lakini wanataka kufanya umakini kumpata kocha mpya na si kukurupuka.