Shabiki atoa simu kama dhamana kuiona Yanga

CHEZEA Yanga wewe! Kuna ushabiki mwingine ni balaa, unaambiwa mwenye banda mwenyewe, Dulla Juma amebaki mdomo wazi baada ya jamaa huyo kuweka dhamana ya simu kwa madai amesahau kubeba kiingilio.

Kwa kuwa mwenye banda ni mtu wa soka, unaambiwa ilibidi aishikilie ile simu baada ya shabiki huyo kujieleza wakati wa mapumziko atarudi haraka ofisini kwake na kwenda kuchukua pesa yake ya kiingilio kisha atarudishiwa simu yake.

Tukio hilo limetokea Gongo la Mboto karibu na kituo cha mabasi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara baina ya Yanga dhidi ya Biashara United.

Kama ambavyo alitoa ahadi, wakati wa mapumziko jamaa alienda fasta kwenye kibanda chake cha biashara na kurejea na jero kisha akarudishiwa siku yake ya mkononi.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ambao ulichezwa Uwanja wa Benjamini Mkapa, shabiki huyo aliondoka kiroho safi bandani baada ya kumalizika kwa dakika 90 huku chama lake likiibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Yacouba Sogne.


Je!! Huko kuna vaibu kama lote? Basi tupe mwaliko kupitia namba

0713-085905 au 0734-035599 ili wazee wa vibanda umiza, Eliya na Mtupa tuje kuliamsha...