Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pablo: Tatizo hawajiamini

Pablo: Tatizo hawajiamini

WAKIONEKANA wachovu huku wakiwa na sura za huzuni, nyota wa kikosi cha Simba walitua jana na kupokewa kwa kejeli na mashabiki wachache wa Yanga, huku kocha Pablo Franco akisema aliwapiga chini mastraika wake kwa vile wamepoteza kujiamini.

Mashabiki hao wa Yanga walikuwa wakiwatania nyota hao wa Simba wakilitaja jina la Hamis Kiiza aliyeiua timu hiyo mjini Bukoba juzi katika mechi dhidi ya Kagera Sugar.

Tofauti na amshaamsha zilizozoeleka kwa mashabiki wa uwanja wa ndege kuwashobokea mastaa wa Simba, jana hali ilikuwa tofauti na kejeli za mashabiki waliokuwa wakihoji alipo Kiiza zilimfanya Ofisa Habari, Ahmed Ally kuingia kati na kujibu; “Anakuja kufanya nini Dar, kwao si Kagera huko, mbona mnateseka hivyo jamani?”

Licha ya mashabiki wa Yanga, kuonekana kuwapopoa wachezaji wa Simba kwa maneno ya shombo, lakini kutokana na ustaarabu wa Ahmed walimuomba wapige naye picha.

Kocha wa Simba, Pablo Franco alisema alichokifanya juzi kwa kutowapanga mastraika na kuwatumia viungo tu, ni kutokana na kumuangusha kwenye mechi kadhaa na alitaka kutumia viungo.

Pablo alisema mastraika hao watatu ni kama walipoteza hali ya kujiamini ndio maana kwenye mazoezi waliamua kubadili mbinu na kutumia mfumo huo wenye (false number nine).

Alisema kuwaweka benchi aliamini wakiingia uwanjani kuna kitu watataka kumuonyesha na kujituma zaidi kwa kufunga mabao kwani hicho ndio kikubwa anachohitaji kutoka kwao.

“Ukiangalia timu yangu katika kila mechi tunatengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao kutoka kwa viungo, mabeki na mawinga ila shida ni kufunga bao,” alisema Pablo na kuongeza;

“Baada ya kuanza na false number nine, tulifanikiwa katika kuendelea kutengeneza nafasi za kufunga, tena zilikuwa zaidi ya nane lakini bado shida ipo pale pale kushindwa kuweka mpira wavuni.”