Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Okwi, Ajibu wakisoma hii ni balaa tupu!

Muktasari:

  • Licha wa washambuliaji mbalimbali wa Ligi Kuu Bara kufurukuta kwenye safu ya ufungaji bora, mshambuliaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, Abdallah Juma ametoa maneno mazito juu ya wachezaji hao.

Dar es Salaam. Yule straika mkali wa mabao aliyetingisha miaka ya nyuma, Abdallah Juma 'Dulla' ameongea maneno makali  ambayo kama washambuliaji kama,  Emmanuel Okwi, Meddie Kagere wa Simba, Ibrahim Ajibu na Mkongo Haritier Makambo wa Yanga watasikia, ni tabu.
Dula mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar na Taifa Stars,  tangu afunge mabao 25, msimu wa mwaka 2006, sasa ni zaidi ya miaka 10, hakuna straika aliyeifikia.
Amesema, anaona washambuliaji wanasifiwa kutokana na kasi zao lakini yeye  bado hajaona  mkali.
"Nasema hivyo kwa sababu tatizo la washambuliaji wa sasa hivi, anafunga mechi moja anakaa mechi tatu na zaidi ndiyo anakuja kufunga tena jambo ambalo si sawa,"alisema Dulla.
Mshambuliaji huyo mwenye asili ya Zanzibar amekwenda mbali zaidi na kusema, anaweza akagundua uwezo wa mshambuliaji bora ni yule atakayeendelea na kasi hiyo kuanzia mzunguko wa 15, na kuendelea.
"Unaweza kusema, Okwi lakini si umeona amefunga mabao matatu mechi moja, baada ya hapo anapotea asifunge tena mpaka mechi tatu kama ilivyokuwa kwa Kagere ambaye alianza zivuri,"alieleza.
Kauli ya Dulla imewaunganisha, Okwi raia wa Uganda, Kagere ambaye ni Mnyarwanda , Ajibu na Mkongo Makambo kwa sababu ndiyo wanaelewa kwa ubora kwenye Ligi Kuu Bara.
Okwi na Eliud Ambokile wa Mbeya City ndio vinara wa mabao kwenye safu ya wafungaji bora, wakiwa wamefunga saba kila mmoja, wanafuatiwa na Habibu Kyombo wa Singida na Said Khamis wa Mbao FC wao wamefungana pia kila mmoja akipachika matano.


Mwaka 2006,  Abdallah Juma mabao 25 (Mtibwa Sugar)
Mwaka 2007-2008, Michael Katende mabao 11 (Kagera Sugar )
Mwaka 2008-2009, Boniface Ambani mabao 18 (Yanga)
Mwaka 2009-2010, Mussa Hassan 'Mgosi' mabao 18 (Simba)
Mwaka 2010-2011, Mrisho Ngassa mabao 18 (Azam)
Mwaka 2011-2012, John Bocco mabao 19 (Azam FC)
Mwaka 2012-2013, Kipre Tcheche mabao 17 (Azam FC)
Mwaka 2013-2014, Amissi Tambwe mabao 19 (Simba)
Mwaka 2014-2015, Simon Msuva mabao 18 (Yanga)
Mwaka 2015-2016, Amissi Tambwe mabao 21 (Yanga)
Mwaka 2016-2017, Simon Msuva (Yanga), Abdulrahman Mussa (Ruvu

Shooting) mabao 14
Mwaka 2017-2018, Emmanuel Okwi mabao 20 (Simba)