Ngushi tena kuwavaa Dodoma Jiji

Muktasari:
Huu ni mchezo wa kwanza kwa Mbeya Kwanza kucheza nyumbani baada ya kucheza mechi mbili ugenini na kukusanya alama nne.
Mbeya.Baada ya kufanya kweli katika mechi iliyopita, leo tena Straika Chrispin Ngushi amepangwa kuanza wakati Mbeya Kwanza ikijiandaa dakika chache kuwavaa Dodoma Jiji.
Ngushi anayecheza Ligi Kuu kwa mara ya kwanza, katika mchezo uliopita alikuwa moto mkali akiisaidia timu yake kusawazisha mabao mawili ya haraka dhidi ya Mbeya City.
Hata hivyo Kinda huyo baada ya kufunga bao la pili la kideoni katika mechi hiyo, alionekana kuumia wakati akishangilia kwa kuruka sarakasi na kuamsha wasiwasi kwa mashabiki wa timu hiyo.
Leo nyota huyo amepangwa tena kuanza katika kikosi cha kwanza chini ya Kocha wake, Hererimana Haruna wakicheza mchezo wao wa kwanza nyumbani katika dimba la Sokoine jijini Mbeya.
Hadi sasa Ngushi ni miongoni mwa wachezaji watatu wenye mabao mawili wakikaa usukani katika orodha ya wafungaji bora baada ya michezo mitatu ya Ligi Kuu.
Kikosi hiki
Hemed Kadedi, Miza Christom, Salum Chuku, Geofrey Rafael, Joseph Majagi, Deogratius Ambakisye, Willy Edgar, Jimy Shoji, Oscar Mwajanga, Paul Peter na Chrispin Ngushi.
Benchi wapo, Rajabu Kaumbu, Baraka Maranyingi, Brown Mwankemwa, Roland Msonjo, Chesco Mwasimba, Mohamed Kapeta, Elisha Anthony, Amis Kanduru na Emanuel Sabinus