Ndayiragije akipangua kikosi chake

Muktasari:
Azam inahitaji ushindi wowote kuvuka hatua inayofuata ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Fasil Kenema ya Ethiopia.
KOCHA Mkuu wa Azam FC, Etienne Ndayiragije amefanya mabadiliko matatu Katika kikosi chake akihitaji ushindi tu kuivusha timu yake.
Azam ambao wanarudi nyumbani dhidi ya Fasil Kenema baada ya kupoteza kwa bao 1-0 ugenini Ndayiragije hajafanya mabadiliko yoyote katika safu yake ya ulinzi ambapo ameanza na kipa Razack Abalora beki wa kulia Nicholas Wadada, kushoto akiwa Bruce Kangwa wakati mabeki wa kati wakiwa Daniel Amoah na Yakubu Mohamed.
Mabadiliko makubwa Ndayiragije ameyafanya katika safu yake ya kiungo akimuanzisha Frank Domayo na Emmanuel Mvuyekure walicheza sambamba na Salum Aboubacar 'Sure Boy'.
Viungo hao wanachukua nafasi ya Oscar Masai aliyeanzia benchi na Abdallah Masoud ambaye hayumo kabisa.
Katika safu ya ushambuliaji Ndayiragije amemuongeza mshambuliaji Dally Ella aliyechukua nafasi ya Salmin Hoza aliyeanzia benchi mshambuliaji huyo akianza sambamba na Obrey Chirwa na Idd Seleman ambao wanaendelea baada ya kucheza mchezo wa kwanza.
Katika benchi Azam itakuwa na kipa Mwadini Ally, beki akiwa Masai,viungo wakiwa Hoza na Idd Kipagwile, wakati washambuliaji wakiwa Donald Ngoma, Paul Peter.