Molinga awajibu kwa vitendo

Muktasari:

Usajili wa David Molinga ndani ya kikosi cha Yanga ulibezwa kutokana na muonekano wake, akaja akawapa moyo wa kuendelea kumkandamizi kwa staili yake ya upigaji faulo.

PAMOJA na kwamba straika wa Yanga, David Molinga kubezwa kwenye usajili wake taratibu ameanza kuwaziba midomo kutokana na kufanya kile kilichomleta Yanga.
Molinga ndiye anayeongoza kwenye kikosi cha Yanga akiwa na mabao mawili akifuatiwa na Mrisho Ngassa mwenye bao moja katika mechi mbili walizocheza za Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Ruvu Shooting na Polisi Tanzania.
Katika mechi mbili ambazo Yanga imecheza imevuna pointi moja inamiliki mabao matatu, huku ikitikiswa mara nne kwenye nyavu zao.
Molinga alikuwa anapata kejeli kutokana na aina ya upigaji  faulo ambapo huoneysha mbwembwe nyingi mara anapotaka kupiga mpira.
Katika mechi ya jana Alhamis, Molinga aliuthibitishia umati uliokuwepo uwanja wa Uhuru kushuhudia mtanange kati ya Yanga na Polisi Tanzania kwamba ni fundi wa kupiga faulo.
Bao la tatu la Yanga lilitokana na faulo aliopiga Molinga nje ya 18 ambapo shuti lake liliingia moja kwa moja nyavuni.