Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayele: Tupeni wiki mbili tu

MASHABIKI wa Yanga wanaamini kikosi chao kimesheheni mastaa wa maana wakitaka sasa kuona mataji yanatua lakini Fiston Mayele amewaambia; “Tupeni wiki mbili tu.”

Mayele aliliambia Mwanaspoti, kwa sasa bado hawajakaa pamoja na kutengeneza timu moja, ila wakifanya hivyo kwa wiki mbili hadi tatu timu yao itakuwa tishio zaidi ya ilivyokuwa kwenye Siku ya Mwananchi.

Mayele ambaye Mwinyi Zahera amemtaja kama kati ya wachezaji tishio, alisema wala hawajaumizwa na kupoteza mchezo uliopita, japo matokeo hayo yamewashtua, ila sasa wanakwenda kujiandaa kihalisia kuelekea msimu ujao.

“Mashabiki ni kitu muhimu kwetu wasiumie na matokeo hii ni mechi yetu ya kwanza hatujapata muda wa kutosha, ila tunakwenda kambini kutengeneza timu,”alisema Mayele ambaye kwa mujibu wa wachambuzi wa soka la DR Congo huwa anaanza msimu taratibu na kuchanganya baadae, japo wamemtaja Heritier Makambo kuwa mkali zaidi.

“Kuna wengine wamekwenda kucheza timu za taifa wakirejea makocha wakiifanya kazi yao naamini ndani ya wiki mbili hadi tatu tutakuwa na mabadiliko makubwa,” alisema Mayele.

Akizungumzia ubora wake, Mayele alifichua, licha ya ujuzi wake wa kufunga ila watu wasitarajie kuwa straika wa kusubiri kutengenezewa nafasi.

“Nilipokuwa Congo sikuwa mshambuliaji wakusubiri kutengenezewa nafasi, ila napenda kupambana na kufunga nikiwa kokote, viungo au mawinga wakinitengenezea nafasi ni jambo zuri.

“Nikikosa msaada huwa napambana, nimeambiwa hapa mabeki wanatumia nguvu sana sina wasiwasi kwni naujua ubora wangu.”


JESHI LA UBINGWA

Katika kuhakikisha msimu huu haitoki patumu, mabosi wa Yanga wameunda jeshi maalum la ubingwa lenye vigogo nane, wakiwamo Lucas Mashauri, Davis Mosha, Seif Ahmed ‘Magari’ na Abdallah Bin Kleb.

Kamati ya Utendaji ya Yanga chini ya Mwenyekiti, Dk Mshindo Msolla imeunda kamati mpya ya Mashindano ya klabu hiyo chini ya Mwenyekiti, Rodgers Gumbo, ikiwa na wajumbe wengine ambao mbali na kina BinKleb ni pamoja na, Injinia Hersi Said, Arafat Haji, Hamad Islam na Pelegrinius Rutayunga.