Matasi alibeba Tusker

Sunday June 19 2022
Matasi PIC
By Sinda Matiko

WAKATI bosi wa Kakamega Homeboyz akiendelea kudai kwamba alifanyiwa ile kitu, kipa wa Tusker FC Patrick Matasi zake ni sherehe tu.

Naibu nahodha huyo anasisitiza kuwa kama sio kwa ubora wake pale nyuma, basi hafikiri Tusker wangefanikiwa kutetea taji lao.

Matasi aliyejiunga na Tusker mwanzoni mwa msimu, alitawazwa kuwa kipa bora akinyakua Golden Gloves baada ya kumaliza msimu bila ya kufungwa kwenye mechi 18.

“Tukiambiana ukweli, rekodi hiyo ilitubeba sana sababu mliona ni tofauti ya idadi ya magoli ndio iliyoamua bingwa ni nani kati yetu na wapinzani Homeboyz. Idara ya ulinda lango kusema kweli ilifanya kazi kubwa kwa kuhakikisha hatukupoteza rada hata siku moja. Na ndio sababu tulicheza mechi kibao bila ya kupoteza.” kachocha Matasi.

Tofauti ya magoli manne ndio iliyowapa ubingwa Tusker FC baada yao kutoshana alama na Homeboyz, kila mmoja akizoa pointi 63 baada ya raundi zote 34.

Clean sheet 18 za Matasi zilihakikisha kuwa Tusker wanaongoza kwa timu iliyofungwa idadi chache za magoli wakipachikwa 17 tu ikilinganishwa na 33 walizofungwa Homeboyz. Kati ya magoli yao 42 walizofungwa ikilinganishwa na 54 za Homeboyz, 11 zilifungwa na straika wao Mtanzania Joshua Ibrahim aliyeibuka mfungaji wao bora.

Advertisement
Advertisement