Masau Bwire aibukia JKT Tanzania

Muktasari:

  • Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa JKT Tanzania, Kapteni Speratus Lubinga alisema wameamua kumrudisha timu kwa wananchi ndio maana wameamua kumpa nafasi Bwire kwaajili ya kuzizungumzia timu zao zote.

TIMU ya kujenga taifa (JKT Tanzania) imemtangaza aliyekuwa Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire kuwa msemaji mkuu wa timu hiyo inayotarajia kucheza Ligi kuu bara msimu wa 2023/24.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa JKT Tanzania, Kapteni Speratus Lubinga alisema wameamua kumrudisha timu kwa wananchi ndio maana wameamua kumpa nafasi Bwire kwaajili ya kuzizungumzia timu zao zote.

Bwire kuanzia leo (jana) atakuwa Msemaji mkuu wa JKT Queens na JKT Tanzania hii ni kwasababu ni mwalimu na mzoefu kwenye masuala ya mpira hivyo atatusaidia kuzizungumzia timu zetu ambazo zina malengo ya kufanya vizuri msimu ujao;

“JKT Queens ndio mabingwa msimu ulioisha wanaenda kushiriki Cecafa na JKT Tanzania imepanda ligi hivyo mambo yote kushuka timu zetu yatazungumzwa kikamilifu na Bwire.” alisema.

Wakati huohuo Bwile aliushukuru uongozi kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo huku akiweka wazi kauli mpya ya ligi hiyo kuwa ni wataoa Kichapo cha kizalendo.

“Naizungumzia timu ambayo ni mabingwa wa Ligi ya wanawake JKT Queens ambayo inaendelea na maandalizi Kigamboni na JKT Tanzania ambayo inashiriki ligi kuu bara msimu ujao baada ya kupanda;

“Tumefanya usajili mzuri ambao utatoa chachu ya ushindani na ndio maana tumekuja na kauli mbiu ya KK ambayo ni kichapo cha kizalendo.” amsema Bwire.