Kibu kuwamaliza mabosi wake

Monday January 17 2022
Kikosi PIC
By Saddam Sadick

Mbeya. Straika Kibu Denis kwa mara ya kwanza leo atakutana na waliokuwa mabosi wake wa zamani baada ya kupewa nafasi ya kuongoza eneo la ushambuliaji kuimaliza Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa hapo baadaye.

Denis ambaye aliitumikia Mbeya City msimu uliopita, leo pamoja na nyota wengine atakuwa na shughuli pevu kuthibitisha ubora wake kuhakikisha anaisaidia timu hiyo kuondoka na alama tatu.

Kikosi kilichowekwa hadharani cha Wekundu chini ya Kocha wake, Pablo Franco ni pamoja na Aish Manula, Shomari Kapombe, Henock Inonga, Joash Onyango, Mohamed Hussein, Mzamiru Yassin, Jonas Mkude, Sadio Kanoute, Benard Morrison, Chris Mugalu na Kibu Denis.

Benchi wapo Beno Kakolanya, Israel Naenda, Paschal Wawa,Pape Sakho, Maddie Kagere, Jimmyson Mwanuke, John Bocco, Hassan Dilunga na Kennedy Juma.

Advertisement