Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam yabanwa dakika 45

Muktasari:

Katika mchezo uliopita Azam walishinda 5-0 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Nyamagana, Mwanza.

KOCHA wa Azam Fc, Aristica Cioaba amefanya marekebisho katika kikosi chake maeneo manne kwenye mchezo wao wa leo Jumamosi unaonedelea Uwanja wa Uhuru jiji Dar es Salaam dhidi ya Alliance ya jijini Mwanza.
Cioaba alifanya mabadiliko upande wa golikipa kwa kumwanzisha Benedict Haule huku mchezo wao dhidi ya Simba uliomalizika wakipoteza 3-2 alimuanzisha Razack Abarola.
Nafasi ya beki wa kati amewaanzisha Daniel Amoah na Oscar Masai wakati mechi iliyopita walianza Yakub Mohamed na Aggrey Morris na eneo la kiungo amemwanzisha Mudathir Yahya na Frank Domayo badala ya Salum Abubakary na Bryson Rafael walioanza mchezo uliopita.
Mabadiliko hayo yameonekana kuwa na tija baada ya maeneo yote kuwa na utulivu tofauti na mchezo uliopita ambapo safu ya viungo ilionekana kukosa utulivu hali iliyowafanya viungo wa Simba watambe na kucheza kwa uhuru watakavyo.
Lakini katika mchezo huu Domayo na Mudathir wamecheza kwa kuelewana kwa kukaba kwa pamoja pia kupiga pasi za mwisho kwa wapinzani.
Eneo la ushambuliaji licha ya mchezo huu kucheza Shabaan Chilunda pekee yake tofauti na ule uliopita akicheza na Obrey Chirwa, Chilunda alishindwa kutamba.
Kocha huyo amelazimika kufanya mabadiliko ya kumtoa Chilunda kipindi cha pili na kumuingiza Andrew Simchimba kwenda kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji ingawa hadi wanakwenda mapumziko hakuna aliyetikisa nyavu za mwenzake.