Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

arsenal VIGEUGEU

Muktasari:

Tofauti na ilivyozoeleka siku za karibuni ambapo mashabiki hao walikuwa wakibeba mabango ya ‘Wenger Out’, jana mambo yalikuwa tofauti huko Emirates wakati Wenger alipokiongoza kikosi chake kwa mara ya kwanza tangu alipotoa kauli za kuachia ngazi mwisho wa msimu. Arsenal ilicheza na West Ham United na kushinda 4-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, huku straika Alexandre Lacazette akipiga mbili.

LONDON, ENGLAND

AMA kweli maisha bila ya unafiki hayaendi. Ndicho unachoweza kusema kuhusu maisha ya Arsene Wenger huko Arsenal baada ya mashabiki wa timu hiyo jana Jumapili kubeba mabango ya kumpongeza kocha huyo siku chache tu baada ya kutangaza kwamba ataachia ngazi mwisho wa msimu.

Tofauti na ilivyozoeleka siku za karibuni ambapo mashabiki hao walikuwa wakibeba mabango ya ‘Wenger Out’, jana mambo yalikuwa tofauti huko Emirates wakati Wenger alipokiongoza kikosi chake kwa mara ya kwanza tangu alipotoa kauli za kuachia ngazi mwisho wa msimu. Arsenal ilicheza na West Ham United na kushinda 4-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, huku straika Alexandre Lacazette akipiga mbili.

Katika mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki 59,422, Arsenal ilitangulia kufunga kupitia kwa Nacho Monreal katika dakika 51, lakini dakika 13 baadaye, West Ham walichomoa kupitia kwa staa wao, Marko Arnautovic.

Wakati mechi ikionekana kama itamalizika kwa sare hiyo ya 1-1, Arsenal ilitumia vyema dakika nane za mwisho kufunga mabao matatu, yaliwekwa wavuni na Aaron Ramsey katika dakika 82 na Lacazette kufunga mara mbili katika dakika 85 na 89.

Katika mchezo huo, mashabiki walibeba mabango yenye maneno matamu kwa Wenger, jambo ambalo lilikuwa tofauti kwa wiki za karibuni.

Mechi hiyo ilikuwa kama send-off kwa kocha Wenger, ambaye hatakuwa na kikosi hicho kwa msimu ujao baada ya kudumu kwenye timu hiyo kwa karibu miaka 22.

Wenger alitangaza kung’atuka wiki iliyopita, lakini taarifa za ndani zinafichua kwamba Mfaransa huyo ametimuliwa baada ya kudaiwa kwamba atalipwa fidia ya Pauni 11 milioni kufidia mwaka mmoja uliobaki kwenye mkataba wake.

Ushindi huo unaifanya Arsenal kushinda mechi yao ya 17 msimu huu na kukusanya pointi 57 baada ya kushuka uwanjani mara 34.

Imetoka sare mara sita na kuchapwa kwenye mechi 11 na kujikuta wakishika nafasi ya sita kwenye msimamo, pointi 11 pungufu ya kuifikia Tottenham Hotspur inayoshika nafasi ya nne, ambayo inatoa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Mchezo mwingine wa ligi hiyo uliofanyika jana, Stoke City walishindwa kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani wa Britannia baada ya kubanwa na Burnley na kutoka sare ya 1-1.

Stoke walihitaji pointi tatu za kuwatoa kwenye hatari ya kushuka daraja, walianza vizuri na kutangulia kwa bao la Badou Ndiaye, lakini Burnley walikuja kuchomoa kupitia kwa Ashley Barnes na kuwaweka pagumu.