YANGA imetinga fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 leo dhidi ya Simba.
Bao pekee la ushindi ambalo limeipekeka Yanga fainali limefungwa na kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' kwa shuti kali la mbali mnamo dakika ya 25 na kudumu kwa dakika zote 90 za mchezo huo.