YANGA imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mbeya Kwanza kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na kufanya kubakiza alama sita pekee ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
Ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha pointi 63 baada ya mechi 25 za ligi huku ikihitaji alama sita kwenye mechi tano zilizobaki ili kuwa bingwa kwani itafikisha jumla ya pointi 69 ambazo hakuna timu yeyote itazifikisha baada ya mechi zote kumalizika.
FT: Yanga 3-0 Mbeya Kwanza
⚽️' 34, F Mayele
⚽️' 39, S Ntibazonkiza
⚽️' 44' D Ambundo.
⚽️' 74' H Makambo