YANGA inaendelea kunusa Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC baada ya leo Jumamosi ya Aprili 23 kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kuvunja mwiko wa kutoifunga Namungo kwenye mechi tano mfululizo za ligi.
Yanga imecheza mechi 20 imeshinda 17, sare tatu dhidi ya Mbeya City, Simba na Namungo, hivyo imefikisha pointi 54.
Mabao ya mchezo huo yalifungwa na Fiston Mayele dakika ya 17, Shiza kichuya dakika ya 33na Feisal Salum dakika ya 39.