Nyota wa tenis, Rafael Nadal ameshinda taji la 21 la Grand Slam Jumapili ya Januari 30, 2022 baada ya kutoka kwa seti mbili na kumduwaza Daniil Medvedev wa Urusi na kushinda Australian Open.
Kwa ushindi huo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 amewapita Roger Federer na Novak Djokovic katika orodha ya wachezaji wa kiume waliocheza nafasi ya juu na kuwa mchezaji wa kwanza wa kiume kushinda zaidi ya mataji 20 ya Grand Slam.