Yametimia, hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya msanii wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ’Harmonize’ kumvalisha pete ya uchumba msanii wa Bongo Movie, Kajala Masanja.
Tukio hilo limefanyika leo Jumamosi Juni 25, 2025 hoteli ya Serena na kulipa jina la ‘Late Lunch’ huku likihudhuriwa na watu wa karibu wa wasanii hao ukiwemo uongozi wa lebo ya Konde Gang, Mkurugenzi wa TV E, Francis Ciza ’Majizo’.
Akizungumza kabla ya kumvalisha pete, Harmonize amesema wamepitia mengi na msanii huyo na anashukuru hatua hiyo waliyofikia.