STRAIKA WA MWANASPOTI: Hivi mnajielewa kuchezesha waliozidi umri?

NDUGU zanguni nimekuwa katika fani ya michezo tangu kuzaliwa kwangu na kwa kweli kuna vitu vingi tuu ambavyo kwa kweli nikitazama vile vinaendeshwa karne hii nashangaa saana.

Leo nitagusia masuala ya kutumia wachezaji katika mashindano kadhaa wachezaji kwa kweli sio wa klabu hiyo ama shule hiyo.

Nimekuwa nikitazama mashindano kati ya shule humu nchini na kweli nasikitika sana wakati naona kuna wachezaji wengi tuu ambao wanatumika katika mashindano hayo ambao hawafai kabisa kutumiwa.

Utapata shule iko na zaidi ya wanafunzi watano ambao wote hao sio wanafunzi wa shule hiyo. Utapata aidha walikuwa wanasoma katika shule hiyo wakamaliza masomo yao ama ni wanafunzi katika shule jirani. Inaudhi sana kwa sababu ukiangalia hapo, tunajenga nini?

Ni aibu sana kuchezesha wachezaji amabo ndani ya roho yako unajua kuwa sio wanafunzi wako ama sio wachezaji wako. Tunajenga nini? Hii unataka kuniambia sio ufisadi?

Kwa mfano tuu kumekuwa na mashindano ya shule za msingi nchini Kenya juzi tuu mashindano ambayo yalimalizika juzi jijini Eldoret. Ukiangalia timu zote zilizo shiriki nitakuambia wazi kuwa timu hizo zote zilikuwa na wachezaji ambao sio wa hizo shule. Ni nini tunakuza hapa.

Wachezaji wengine tayari walikuwa washapitisha miaka ya kushiriki katika mashindano hayo. Wachezaji wengine tayari washaa maliza shule wamerejeshwa kuja kucheza soka tuu.

Hii ni uzembe mtupu na kwangu nasisitiza kuwa Shirikisho la Soka Kenya (FKF) ni lazima wazingatie na waweke sheria kabambe ambazo zitaweza kumaliza ujinga kama huu usiendelee.

Kwangu wachezaji kama hao nawaita Mamluki kwa sababu naona kwa kweli hawana tofauti na mamluki.

Itakuwaje wewe ulimaliza shule kidato cha nne miaka miwili mitatu iliyopita na bado unachezea shule hiyo?

Kakazangu huu ni wizi mtupu. Na sio Shule za misingi ama za sekondari pekee jambo hili linafanyika. Ni mambo ambayo yanafanyika kila sekta ya michezo.

Inaudhi sana kutumia wachezaji ambao wewe unafahamu kuwa sio wako ama unafahamu kuwa washaa pitia umri fulani.

Kwanza katika soka letu kumekuwa na udanganyifu mkubwa saana haswaa ikija upande wa umri wa wachezaji. Utapata mchezaji umri wake kamili ni miak 23 lakini anabaki akidanganya watu kuwa yupo na miaka 18. Jambo amablo linaathiri hadi timu setu za kitaifa haswaa timu za vijana wasiozidi miaka Ishirini kurudi chini.

Kenya tumejipata tukipigwa faini na kubanduliwa mashindanoni kwa sababu ya kuchezesha wachezaji ambao tayari washapita umri. Wakati uchunguzi unapofanywa inapatikana kuwa hao wachezaji umri wao ushaa pita. Iko shida gani ya sisi kuweza kutengeneza timu bila kupitia mikato ndugu zanguni.

Inaudhi sana na shirikisho la kandanda ni lazima lizingatie kuweka mikakati sambamba. Kuanzia shule za primari hadi shule za upili. Sio vyema unapata timu fulani iko na vijana wachanga saaana hata ukiangali kisura ni watoto tuu unapata wanacheza dhidi ya majibaba wengi tayari hata wanafaa kuwa washaa anzaa kujenga familia nabado wanajishughlisha na soka la watoto.

Ni tabia ambayo tunafaa kuikemea vilivyo kama nchi. Hapo tuu ndio tutakuza vipaji vyetu vizuri tuu bila shida yoyote.

Timu zetu za kitaifa za watoto wasiozidi umri wa miaka 20 imejaa wachezaji wenye wapo zaidi ya miaka 22,23. Timu za vijana wa miaka 18 imejaa wachezaji ambao tayari washaa pitisha hizo miaka.

Tunaenda wapi kisoka. Shule zingine za sekondari kakangu kuna wanafunzi wengi wanazunguka tuu hizo shule. Mara leo yuko Kakamega High,Msimu ujao Barding,Msimu ujao yuko Musingu,msimu unafata yuko Chesamisi, baada ya msimu miwili yuko Sirakalu high school.

Kwani huyu mwanafunzi hamalizi shule? Haiya basi kama hata hamalizi shule miaka zake kwani hazisongi jameni?

Haiwezekani. Kwa hivyo naomaba shirikisho la soka liweze kuweka mikakati kabambe kuanzia shule za misingi,hadi za upili kisa na maana hapo ndipo kuna wizi mkubwa kakazangu.

Iwapo tutazingatia maswala haya ndugu zanguni mbona tusiende kombe la dunia bila wasiwasi. Ni mikakati za ukweli.

Data ya wachezaji hawa kuanzia shuke za misingi iwekwe. Hapo tutajua ni yupi anadanganya umri na yupi yupo sawa.

Bila hivyo itakuwa hekaya za abunwasi. Tutakuwa tunatolewa mashindanoni kila mwaka juu ya udanganyifu wa miaka. Hapo hakuna soka tutakuwa tunakuza.